LONDON, England
KWA ushindi wa ‘KO’ ya raundi ya tano dhidi ya Daniel Dubois, Oleksandr Usyk amevuna Pauni milioni 98 (zaidi ya Sh bil. 343 za Tanzania).
Pambano hilo la uzito wa juu lilipigwa jana katika Uwanja wa Wembley.
Usyk, raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 38, alimdunda Dubois na kuendeleza rekodi yake ya kutokupoteza pambano.
Kwa ushindi huo, sasa Usyk anashikilia mikanda yote mikubwa ya dunia, kwa maana ya IBF, WBA (Super), WBO na WBC.
Wakati bondia huyo akiondoka na Pauni milioni 98, Dubois amelipwa Pauni milioni 53 (zaidi ya Sh Bil. 185).
Published:


