LOS ANGELES, Marekani
MASTAA wa tenesi, Jannik Sinner na Novak Djokovic, hawatoshiriki michuano ijayo ya National Bank Open itakayofanyika Canada.
Wawili hao walitarajiwa kushiriki mashindano hayo ya kwanza makubwa tangu yalipomalizika yale ya Wimbledon.
Kuelekea michuano hiyo ya wiki ijayo, leo waandaaji wake wamekuja na taarifa ya kuwakosa nyota hao.
“Jannik Sinner na Novak Djokovic wamelazimika kujitoa kwenye michuano ya mwaka huu ya National Bank Open itakayofanyika Toronto ili waweze kujiweka sawa baada ya Wimbledon.
Katika taarifa hiyo, pia waratibu hao waliweka wazi kuwa watamkosa staa mwingine wa tenesi, Jack Draper, ambaye anasumbuliwa na majeraha.
Published:


