MERSEYSIDE, England
MABOSI wa Everton wanakaribia kutangaza mkataba mpya wa miaka minne mlinda mlango wao raia wa England, Jordan Pickford.
Pickford mwenye umri wa miaka 31, atasaini mkataba huo, licha ya huu wa sasa kuwa umebakiza miaka miwili.
Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa mkataba mpya huo utamfanya kipa huyo kupandishiwa mshahara anaolipwa sasa wa Pauni milioni sita kwa mwaka.
Licha ya ubora wake na kuhusishwa mara kadhaa na vigogo, Pickford amesisitiza kuna anataka kubaki Everton, klabu aliyoitumikia katika michezo 320 ya Ligi Kuu ya England (EPL).
Kwa nyakati tofauti, Pickford aliweza kuwania namba na Nick Pope, Aaron Ramsdale, Dean Henderson na Sam Johnstone, lakini ameendelea kuwa chaguo la kwanza klabuni hapo.
Published:


