LAS VEGAS, Marekani
MKONGWE wa ndondi za uzito wa welter, Manny Pacquiao, amesema anatamani kuona akirudiana na bingwa wa WBC, Mario Barrios.
Pacquiao mwenye umri wa miaka 46, ameibuka na kauli hiyo baada ya kupata sare katika pambano lake na bondia huyo.
Ikiwa ni miaka minne imepita tangu alipopanda ulingoni, bado Pacquiao alionekana kuhimili vishindo vya mpinzani wake huo kwa muda wote wa pambano lao.
Akizungumza baada ya pambano, Pacquiao ambaye ni bingwa wa mikanda 12, alisema anaamini alishinda pambano hilo.
“Nafikiri nilishinda,” alisema Pacquiao na kuongeza: “Mpinzani wangu alikuwa bora, lilikuwa ni pambano zuri.”
Pacquiao anaendelea kushikilia rekodi ya bondia mwenye umri mkubwa zaidi kubeba ubingwa wa welter, alipofanya hivyo akiwa na miaka 40 mwaka 2019.
Published:


