LONDON, England
KOCHA mpya wa Tottenham, Thomas Frank, hajawahi kufukuzwa kazi lakini sasa anahofia kuipoteza rekodi hiyo.
Frank raia wa Denmark, anakuwa kocha wa 14 kwa miaka ya hivi karibuni ndani ya klabu ya Tottenham.
Kwa miaka saba akiwa kocha wa Brentford, Tottenham imewafungashia virago makocha watano.
Kwa upande wake, Frank amekiri kuwa huenda Tottenham ikawa klabu ya kwanza kumfuta kazi.
“Kuja kwenye klabu kubwa huwa kuna presha. Tunapaswa kufanya vizuri kwa sababu ni jukumu letu sote; mimi, wafanyakazi, wachezaji, na kila mmoja wetu. Ni jukumu letu kwa Pamoja,” alisema.
Published:


