LONDON, England
KLABU ya Arsenal imefanikiwa kuinasa saini ya winga wa kimataifa wa England, Noni Madueke.
Arsenal imemng’oa nyota huyo Chelsea, huku usajili huo ukiripotiwa kugharimu kiasi cha Pauni milioni 48.5.
Madueke (23), alikuwa sehemu ya kikosi cha Blues kilichokuwa Marekani kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu lakini alirudi mapema jijini London ili kukamilisha dili lake na Arsenal.
Staa huyo amesaini mkataba wa miaka mitano Emirates. “Nimefurahi kuwa hapa. Nawashukuru nyote mliofanikisha,” alisema.
Ameondoka Chelsea akiwa ameitumikia katika michezo 92 tangu ilipomsajili akitokea PSV Eindhoven kwa ada ya Pauni milioni 30 mwaka 2023.
Anakuwa mchezaji wa nne kusajiiwa na Arsenal majira haya ya kiangazi baada ya Kepa Arrizabalaga, Christian Norgaard na Martin Zubimendi.
Published:


