12.5 C
New York

Newcastle: Isak haendi Liverpool

Published:

LONDON, England
MABOSI wa Newcastle United wameweka mgomo wakisisitiza kuwa mpachikaji mabao wao, Alexander Isak, hauzwi kwa gharama yoyote.
Newcastle wamedai kuwa hata kama nyota huyo anaitaka Liverpool, wao hawako tayari kukaa mezani na klabu hiyo ya Merseyside.
Isak ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita, anatajwa kuwa na thamani ya Pauni milioni 120.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Newcastle United, Yasir Al-Rumayyan, ameweka wazi kuwa staa huyo hauzwi hata kwa dau litakalovunja rekodi ya usajili nchini Uingereza.
Wakati huo huo, Al-
Rumayyan amefichua kuwa bado wanaamini Isak atasaini mkataba mpya, hasa baada ya kumpa ofa ya mshahara mkubwa zaidi ya huu wa sasa wa Pauni 130,000 kwa wiki.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img