12.5 C
New York

Mtoto wa Ancelotti ‘aula’ Brazil

Published:

RIO, Brazil
DAVIDE Ancelotti ambaye ni mtoto wa kocha Carlo Ancelotti, amekabidhiwa mikoba ya kuinoa Botafogo ya Ligi Kuu ya Brazil.
Davide amekuwa na kikosi hicho tangu kiliporejea kutoka katika michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Katika mashindano hayo, Botafogo walifika hatua ya 16 bora, wakiondoshwa na Wabrazil wenzao, Palmeiras.
Mbali ya kibarua hicho, bado Davide ataendelea kuwa msaidizi wa baba yake, Ancelotti, katika majukumu ya kuinoa timu ya taifa ya Brazil.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img