MANCHESTER, England
MABOSI wa Manchester United wamelazimika kurudi kwa mara ya tatu kwa Brentford wakijaribu kuishawishi kumwachia Bryan Mbeumo.
Kwa mujibu wa ripoti mpya, safari hii Man United wamefika mezani wakiwa na ofa ya Pauni milioni 70.
Hatua hiyo imekuja baada ya ofa zao mbili kutupiliwa mbali na mabosi wa Brentford.
Man United wanaamini watainasa saini ya nyota huyo raia wa Cameroon kabla ya kwenda Marekani Jumanne ya wiki ijayo kwa ajili ya ‘pre-season’.
Published:


