LONDON, England
MICHUANO ya soka la wanawake ya EURO 2025 imefikia patamu na sasa England itakwaana na Italia katika hatua ngumu ya nusu fainali.
England ilivuka robo fainali baada ya ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Sweden, mchezo ambao dakika za kawaida zilimalizika kwa sare ya 2-2.
Kwa upande wake, kocha wa England, Sarina Wiegman, amewapongeza Sweden akiwaita kuwa ni wapinzani wagumu kuwahi kukutana nao.
“Ilikuwa ni mechi ngumu kuliko zote nilizowahi kuona. Tulinusurika mara nne au tano,” alisema Wiegman akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
Dhidi ya Italia katika mchezo wa Jumanne ya wiki ijayo, nao ni mtihani mwingine mgumu kwa England.
Italia wameingia nusu fainali kwa mara ya kwanza baada ya kuikosa hatua hiyo tangu mwaka 1997.
Published:


