MOSCOW, Urusi
STAA wa mchezo wa ngumi, Timur Khizriev, ameripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Video iliyosambaa mitandaoni inamuonesha bingwa huyo wa uzito wa feather akivamiwa na watu wawili, kabla ya kupigwa risasi.
Khizriev mwenye umri wa miaka 29, alikutwa na majangwa hayo akiwa kwenye gari lake mjini Makhachkala.
Hata hivyo, ripoti zinaeleza kuwa Khizriev alipata majeraha ya bega, mkono na kifua lakini anaendelea vizuri katika matibabu yake.
Published:


