13.9 C
New York

Kocha United apewa mikoba Oman

Published:

MUSCAT, Oman
ALIYEWAHI kuwa kocha msaidizi wa Manchester United wakati ule wa Alex Ferguson, Carlos Queiroz, ametangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Oman.
Mkufunzi huyo raia wa Ureno ndiye aliyeiongoza Iran kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014 na 201.
Amekabidhiwa Oman wakati huu ikiwa raundi ya nne ya mechi za kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani.
Oman inaunga na mataifa mengine matano (Saudi Arabia, Iraq, Indonesia, Falme za Kiarabu na Qatar) kusaka tiketi ya kwenda kwenye michuano hiyo.
Queiroz aliyechukua nafasi ya Rashid Jaber, ana umri wa miaka 72 na aliwahi kuzinoa Real Madrid na timu za taifa za Ureno, Misri, Colombia na Qatar.
Alifukuzwa kazi na mabosi wa Qatar mwishoni mwa mwaka 2023 baada ya kuinoa timu hiyo katika mechi 11 pekee.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img