RIYADH, Saudi Arabia
KLABU ya Al Nassr ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia imemtangaza Jorge Jesus kuwa kocha wake mkuu.
Ni miezi isiyozidi mitatu tangu Mreno huyo alipoachana na wapinzani wakubwa wa Al Nassr, Al Hilal.
Jesus amesaini mwaka mkataba wa mwaka mmoja na atafanya kazi na Mreno mwenzake, Cristiano Ronaldo, ambaye ni mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho.
Katika hatua nyingine, Jesus mwenye umri wa miaka 70 alisema Ronaldo ndiye aliyesababisha uamuzi wake wa kujiunga na Al Nassr.
“Kama si Cristiano Ronaldo, nisingekuwa hapa. Morali iko juu na Al Nassr inapaswa kubeba mataji …” alisema Jesus.
Ikumbukwe, Jesus anakuwa kocha wa tano kuajiriwa na Al Nassr tangu Ronaldo alipotua klabuni hapo mwishoni mwa mwaka 2022.
Published:


