13.9 C
New York

Isak kuvunja rekodi Liverpool

Published:

MERSEYSIDE, England
LIVERPOOL inaangalia uwezekano wa kufungua pochi na kumsajili mpachikaji mabao wa Newcastle United, Alexander Isak.
Inaelezwa kuwa Liverpool wamepanga kumfanya Isak kuwa mchezaji wa bei mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo.
Hivi karibuni, klabu hiyo ya Merseyside ilivunja rekodi yake ya usajili kwa kumchukua Florian Wirtz aliyegharimu Pauni milioni 116 akitokea Bayer Leverkusen.
Taarifa zinadai kuwa mabingwa hao wa msimu uliopita wa EPL wamemtengea Isak kiasi cha Pauni milioni 125.
Hata hivyo, Newcastle nao wanapambana kumbakiza staa wao huyo, ikielezwa kuwa wamempa ofa ya ongezeko kubwa la mshahara anaopokea sasa wa Pauni 120,000 kwa wiki.
Isak ameshaunga na wachezaji wengine wa Newcastle katika kambi ya ‘pre-season’ waliyoweka Austria.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img