13.9 C
New York

Tolisso aingia rada za Man United

Published:

MANCHESTER, England
MABOSI wa klabu ya Manchester United wameanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa, Corentin Tolisso.
Matheus Cunha kutoka Wolves ni usajili pekee waliofanya Man United majira haya ya kiangazi.
Hata hivyo, ‘Mashetani Wekundu’ hao wametajwa kukaribia kumnasa mpachikaji mabao wa Brentford, Bryan Mbeumo.
Pia, kwa siku za hivi karibuni, Man United imekuwa ikihusishwa na kiungo wa PSG, Fabian Ruiz, na Javi Guerra wa Valencia.
Lakini, kwa mujibu wa gazeti la L’Equipe la Ufaransa, Tolisso ameingia kwenye orodha ya viungo wanaowindwa Old Trafford.
Tolisso, kwa upande wake, ameonesha kuvutiwa na mpango huo wa kujiunga na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Hata hivyo, ripoti zinaeleza kuwa mchezaji huyo hana mpango wa kulazimisha kuondoka Lyon endapo Man United itashindwa kufikia makubaliano na klabu hiyo aliyojiunga nayo akiwa na umri wa miaka 13.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img