13.9 C
New York

Chelsea, Liver zaongoza wa matanuzi sokoni

Published:

LONDON, England
ZIKIWA zimebaki siku 50 kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, klabu za Chelsea na Liverpool ndizo zilizotumia fedha nyingi sokoni.
Chelsea imeshatumia Pauni milioni 211 kuzinasa saini za Essugo, Delap, Sarr, Joao Pedro, Gittens, Estevao Willian na Kendry Paez.
Liverpool wao wameshamwaga Pauni milioni 185 kuwasajili Wirtz, Kerkez, Jeremie Frimpong na Giorgi Mamardashvili.
Tottenham inashika nafasi ya tatu kwa Pauni milioni 122, ikifuatiwa na Manchester City (Pauni mil. 113) na Sunderland (Pauni mil. 100).
Hata hivyo, kufikia hatua hii, Fulham ndiyo klabu pekee ambayo haijatumia kiasi chochote cha fedha kwenye usajili.
Crystal Palace wao wametumia Pauni milioni 2 pekee kumsajili beki kutoka Ajax, Borna Sosa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img