13.9 C
New York

Messi gari limewaka huko Marekani

Published:

MIAMI, Marekani
MSHAMBULIAJI wa Inter Miami, Lionel Messi, ameendeleza makali yake ya kufunga mabao mawili katika kila mchezo, safari hii akiwatungua Nashville.
Messi anakuwa mchezaji wa kwanza kuingia kambani mara mbili katika mechi tano mfululizo za Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
Jana, Inter Miami walikuwa mzigoni kumenyana na Nashville, ambapo Messi alifunga yote katika ushindi wao wa mabao 2-1.
Kufikia hatua hii, Muargentina huyo ndiye kinara wa mabao wa MLS akiwa ameshacheka na nyavu mara 16 katika mechi 16.
Kwa upande mwingine, ushindi wa Jumamosi umeifanya Inter Miami kubaki nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu hiyo.
Inter Miami wamezidiwa pointi tano pekee na Philadelphia waliochimbia kileleni.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img