LONDON, England
MWANAJESHI pekee wa Uingereza aliyekuwa hai tangu alipopigana Vita ya Pili ya Dunia, Donald Rose, amefariki jana akiwa na umri wa miaka 110.
Rose aliyezaliwa mwaka 1914, anatajwa kuwa ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi nchini Uingereza.
Mkongwe huyo mzaliwa wa Westcott, alijiunga na jeshi akiwa na miaka 25 na alihudumu katika kitengo cha ulengaji shabaha.
Wakati wa utumishi wake, alifanya Afrika ya Kaskazini na barani Ulaya.
Inaelezwa kuwa wakati wa Vita ya Pili, Rose, licha ya kunusurika kifo, alipigwa risasi ya mguu.


