LONDON, England
MATAJIRI wa Al Hilal ya Saudi Arabia nao wamejitosa kuiwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko.
Aidha, hiyo inaweza kuwa habari mbaya kwa Arsenal kwani nao wamekuwa wakimfukuzia nyota huyo wa kimataifa wa Slovenia.
Al Hilal wamemgeukia Sesko baada ya Victor Osimhen kukataa ofa zao mbili.
Taarifa zinaeleza kuwa Waarabu hao wamemtengea nyota huyo ofa nono ya Pauni milioni 77 (zaidi ya Sh bil. 270 za Tanzania).
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Saudia msimu uliopita, hivi karibuni walimtangaza Simone Inzaghi kuwa kocha wao mpya baada ya kumng’oa Inter Milan.
Published:


