15.5 C
New York

Napoli na ubabe kwa vigogo Serie A

Published:

NAPOLI, Italia
TANGU iliponunuliwa na bilionea De Laurentiis na kurejea Serie A mwaka 2017, Napoli imekuwa tishio kwa vigogo wa Ligi Kuu hiyo ya Italia.
Msimu uliopita, Napoli ilitwaa taji la Serie A kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu ya hivi karibuni.
Chini ya kocha mzawa, Antonio Conte, Napoli ilinyakua ubingwa ikiwa imeizidi pointi moja Inter Milan iliyoshika nafasi ya pili.
Nje ya uwanja, Napoli ni moja ya klabu zenye uchumi mzuri kwa sasa. Inashika nafasi ya 30 katika orodha ya klabu zenye thamani kubwa duniani.
Mafanikio hayo yametokana na faida nzuri waliyotengeneza ndani ya miaka 10 hadi 15 ya hivi karibuni.
Kwa kumuuza Gonzalo Higuain kwenda Juventus, Napoli ilivuna kitita cha Pauni milioni 75.3).
Pia, PSG ililipa Pauni milioni 59 kumchukua Khvicha Kvaratskhelia, pia Pauni milioni 55 kwa Edinson Cavani.
MASHINE MPYA KUTOKA EPL
Baada ya kumsajili Scott McTominay kutoka Manchester United, Napoli walirudi England na kumchukua mido wa Kibelgiji, Kevin de Bruyne.
Wawili hao wanakutana na Romelu Lukaku na Billy Gilmour, ambao pia waliwahi kukipiga Ligi Kuu ya England.
Katika hatua nyingine, Napoli inajaribu kuinasa saini ya Jack Grealish, pia ikiwatolea macho mastaa wawili wa Man United, Alejandro Garnacho na Jadon Sancho.
WAPINZANI HOI
Inter, baada ya kuonesha upinzani mkali msimu uliopita,
wamepata pigo la kuondokewa na kocha wao, Simone Inzaghi, ambaye ametimkia Al-Hilal ya Saudi Arabia.
Atalanta iliyoshika nafasi ya tatu, nayo imepoteza kocha wake wa muda mrefu aliyewapa taji la Europa miaka miwili iliyopita, Gian Piero Gasperini. Ametua Roma.
Wakati Juventus nao wakiwa bado ‘wanajitafuta’, Napoli inaye kocha mwenye ‘CV’ kubwa, Antonio Conte.
Msimu uliopita, ulikuwa ni ubingwa wake wa tano wa Ligi Kuu ya Italia.
Pia, akaweka rekodi ya kuwa kocha pekee kuwahi kubeba ‘ndoo’ hiyo akiwa na klabu tatu tofauti (Juventus, Inter Milan na Napoli).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img