15.5 C
New York

Bayern: Musiala bado sana kurudi uwanjani

Published:

MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich imethibitisha kuwa mshambuliaji wake, Jamal Musiala, atakuwa nje ya dimba kwa muda mrefu.
Musiala alivunjika mguu wikiendi iliyopita, wakati Bayern ikiumana na PSG katika mchezo wa Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 22, aliumia baada ya kugongana na mlinda mlango wa PSG, Gianluigi Donnarumma.
Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Mercedes-Benz mjini Atlanta ulimalizika wa PSG kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Desire Doue na Ousmane Dembele.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img