LOS ANGELES, Marekani
KLABU za Ligi Kuu ya Marekani (MLS) na zile za Mexico (Liga MX) zinapigana vikunbo kuiwania saini ya mpachikaji mabao wa zamani wa Manchester City na Liverpool, Mario Balotelli.
Mtandao wa TalkSPORT umeeleza kuwa Balotelli mwenye umri wa miaka 34 ni mchezaji huru baada ya kuachana na Genoa na hana mpango wa kustaafu.
Kwa upande wa Mexico, klabu inayomtolea macho ni Cruz Azul, ambayo ilijaribu kumsajili mwishoni mwa mwaka jana.
Marekani nako, klabu ya Los Angeles inaitaka saini ya Balotelli baada ya straika wake, Olivier Giroud, kurejea barani Ulaya na kujiunga na Lille ya Ufaransa.
Ukiacha Balotelli, Los Angeles pia inahusishwa na mpango wa kumsajili mpachikaji mabao wa Bayern Munich, Thomas Muller.
Published:


