TEXAS, Marekani
MVUA kubwa iliyosababisha mafuriko imeondosha uhai wa watu 24, huku wengine 25 wakiendelea kutafutwa.
Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka, wahanga wa majanga hayo ni wakazi wa pembezoni mwa Mto Guadalupe huko Texas, Marekani.
Akizungumzia tukio hilo, Gavana wa Texas, Greg Abbott, alisema zoezi la kuokoa liliendeshwa usiku wa kuamkia leo.
Kwa upande wake, Rais wa Donald Trump alisema Serikali yake itakuwa bega kwa bega na wahanga wote wa tukio hilo.
Published:


