24.7 C
New York

Banda kinara wa mabao WAFCON

Published:

RABAT, Morocco

MSHAMBULIAJI wa kati wa timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ya Zambia, Barbra Banda, ndiye anayeongoza msimamo wa wafungaji bora msimu huu wa fainali za WAFCON (AFCON ya Wanawake).

Michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), imefikia nusu fainali, hatua ambayo itaanza kuchezwa keshokutwa (Jumatano).

Banda mwenye umri wa miaka 26, ameshazipasia nyavu mara tano, akimzidi moja mshambuliaji wa Ivory Coast, Ines Konan.

Hata hivyo, Banda na Konan hawana nafasi ya kuongeza mabao kwani timu zao hazikuweza kufika hatua hii ya nusu fainali.

Katika hatua ya nusu fainali, Algeria watakuwa na kibarua mbele ya Malawi, wakati Morocco wao wataikabili Cameroon.

Nyota wengine walio kwenye orodha ya wafungaji bora kufikia hatua hii ni Thembi Kgatlana (Afrika Kusini), Temwa Chawinga (Malawi) na Marie Ngah (Cameroon), ambao kila mmoja amefunga matatu.

Nyota wenye mabao mawili ni Marine Dafeur (Algeria), Sakina Ouzraoui (Morocco), Uchenna Kanu (Nigeria), Rasheedat Ajibade (Nigeria), na Asissat Oshoala (Nigeria).

Related articles

Recent articles