LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amewapa wiki mbili viongozi wa klabu hiyo kuhakikisha wanamnasa straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres.
Na endapo wataikosa saini ya staa huyo wa kimataifa wa Sweden, basi wapate straika mwingine.
Arteta amekuwa akiweka wazi nia yake ya kuongeza mshambuliaji wa kati, akihusishwa pia mara kadhaa na Benjamin Sesko (RB Leipzig) na Ollie Watkins (Aston Villa).
Hata hivyo, taarifa za hivi karibuni zimekuwa zikieleza kuwa Arsenal wako mbioni kumalizana na Gyokeres.
Kwa mujibu wa taarifa, wameshamalizana na mchezaji huo juu ya masilahi binafsi na sasa wako mezani na klabu yake.
Published:


