LONDON, England
WAKALA wa soka maarufu, Jonathan Barnett, amefunguliwa mashitaka akituhumiwa kwa makosa ya udhalilishaji wa kijinsia.
Barnett (75), ambaye aliwahi kuwasimamia mastaa Gareth Bale na Jack Grealish, anatajwa kujihusisha na biashara ya ‘kuuza’ wasichana kwa ajili ya ngono.
Mbali ya hilo, pia wakala huyo wa kandanda anashitakiwa kwa makosa ya ubakaji na kupiga wanawake.
Aliyefungua kesi ni mwanamke ambaye bado jina lake limehifadhiwa, akidai kuwa Barnett alimsafirisha kutoka Australia hadi Uingereza mwaka 2017.
Akieleza zaidi, mwanamke huyo alisema wakala huyo alimfanya mtumwa wa ngono, ikiwamo kumbaka mara 39.
Wakala wa Bale aingia matatani
Published:


