LUSAKA, Zambia
WATALII wawili, akiwamo raia wa Uingereza, wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na tembo.
Easton Taylor mwenye umri wa miaka 68 na mwenzake raia wa New Zealand, Alison Taylor (67), walivamiwa na tembo huyo walipokuwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya South Luangwa.
Inaelezwa kuwa watalii hao waliishi kwa siku nne katika kambi ya Big Lagoon, umbali wa kilometa 600 kutoka Mji Mkuu wa Lusaka.
“Walikuwa njiani wakielekea katika kambi nyingine, ndipo tembo akawa anawafuata. Tunasikitika kuwapoteza wageni wetu,” ilieleza taarifa ya polisi.
Mwaka jana, watalii wawili raia wa Marekani waliuawa katika matukio mawili tofauti ya kushambuliwa na tembo Kusini mwa Zambia.
Published:


