18 C
New York

Salah akatisha likizo kisa Jota

Published:

MERSEYSIDE, England
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah, amelazimika kukatiza likizo na kurejea Uingereza kutokana na kifo cha mchezaji mwenzake wa klabu hiyo, Diogo Jota.
Kwa mujibu wa taarifa, Salah, kama ilivyo kwa mastaa wengine wa Liverpool, walipaswa kurudi Julai 8, mwaka huu, kwa ajili ya ‘pre-season’.
Jota alifariki jana akiwa na kaka yake, Andre Silva, baada ya gari walilokuwa wakiendesha kuwaka moto, tukio lililotanguliwa na tairi kupasuka.
Inaelezwa, Jota aliamua kutumia usafiri wake baada ya ushauri wa madaktari waliomtaka kutokupanda ndege kutokana na upasuaji wa mapafu aliokuwa amefanyiwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img