15.5 C
New York

Jota, kaka yake wafariki ajali ya gari

Published:

MERSEYSIDE, England
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Diogo Jota, amefariki katika ajali ya gari. Amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 28.
Katika ajali hiyo iliyotokea leo katika Kisiwa cha Zamora nchini Hispania, pia kaka wa mchezaji huyo, Andre Silva, naye amepoteza Maisha.
Kama ilivyo kwa Jota, Silva aliyefariki akiwa na umri wa miaka 26 naye alikuwa mchezaji wa kandanda akiitumikia Penafiel ya Ligi Daraja la Pili huko Ureno.
Kwa mujibu wa mashuhuda, gari lao aina ya Lamborghini liliacha barabara baada ya tairi kupasuka.
Ni siku chache tu zimepita tangu Jota alipofunga ndoa na mpenzi wake wa miaka mingi, Rute Cardoso, na staa huyo wa timu ya taifa ya Ureno ameacha watoto watatu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img