TEHRAN, Iran
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzitambua Israel na Marekani kuwa ni chanzo cha mgogoro unaoendelea.
Huku vita hiyo ikigharimu maisha ya raia wasio na hatia, Israel na Marekani zimeendelea kuishambulia Iran kwa madai ya kuizuia kutengeneza silaha za nyuklia.
Kupitia barua yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres, na Rais wa Baraza la Usalama, Carolyn Rodrigues-Birkett, Araghchi ameomba wapinzani wake hao kuchukuliwa hatua.
Araghchi alienda mbali zaidi na kulitaka Baraza hilo kuzilazimisha Israel na Marekani kulipa fidia kutokana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na vita inayoendelea.


