11.6 C
New York

Staa England adakwa kwa ulevi

Published:

LONDON, England
KIUNGO wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Paul Ince, ameingia matatani baada ya kukutwa akiendesha gari akiwa amelewa.

Ince mwenye umri wa miaka 57, aligundulika baada ya gari lake aina ya Range Rover kupata ajali mjini Cheshire, tukio lililotokea wikiendi iliyopita.

Polisi walifika eneo hilo na kumkamata, kabla ya kumfungulia mashitaka kwa kosa la kuendesha gari akiwa ‘ameutwika’.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na gazeti la Mirror, staa huyo atapanda kizimbani Julai 18, mwaka huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img