NAPOLI, Italia
LICHA ya kuhusishwa na klabu kadhaa za Ulaya, zikiwamo pia za Saudi Arabia, Victor Osimhen ataungana na wachezaji wengine wa Napoli kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao.
Msimu uliopita, Osimhen alicheza kwa mkopo Galatasaray ya Uturuki, ambako ‘alikiwasha’ kwa kufunga mabao 37 na ‘asisti’ nane na kuipa timu hiyo mataji mawili.
Sasa, kwa mujibu wa ripoti, Napoli wamebadili maamuzi ya kumuuza na sasa watamjumuhisha katika kikosi cha ‘pre-season’.
Kabla ya hapo, taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria atafanyiwa vipimo vya afya ifikapo Julai 14, mwaka huu.


