11.6 C
New York

LeBron aiweka njiapanda Lakers

Published:

LOS ANGELES, Marekani
HATUA ya staa wa Angeles Lakers ya Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), LeBron James, kutokuongeza mkataba imeibua minong’ono kuwa huenda staa huyo anafikiria kustaafu.

LeBron (40), amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, hivyo atakuwa mchezaji huru hapo mwakani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2018.

Wakati kukiwa bado kuna sitonfahamu juu ya hatima yake baada ya msimu ujao kumalizika, wapo wanaoamini atatundika daluga na kugeukia uchambuzi wa mechi za NBA.

Mbali ya taaluma hiyo, zipo taarifa pia kwamba kuna ofa zingine za uigizaji, hivyo haitashangaza kuona LeBron akiibukia Hollywood.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img