12.7 C
New York

Kocha Bafana Bafana aita kikosi cha AFCON

Published:

PRETORIA, Afrika Kusini
KOCHA wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, Hugo Broos, ameita
kikosi cha awali cha wachezaji 54 kwa ajili ya fainali zijazo za Mataifa Afrika (AFCON).
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Desemba 21, mwaka huu, kabla ya kufikia tamati Januari 28, mwakani, mwenyeji akiwa ni Morocco.
Kocha huyo raia wa Ublegiji ameita kikosi kikubwa lakini atalazimika kubaki na wachezaji 23 watakaoshiriki AFCON.
Miongoni mwa mastaa waliochomoza katika kikosi cha sasa ni ‘fundi’ wa eneo la kiungo, Themba Zwane.
Zwane ameitwa kikosini, licha ya nyota huyo wa Mamelodi Sundowns kutokucheza mechi yoyote kutokana na majeraha.
Wakati huo huo, kinda wa miaka 20 anayekipiga Club Brugge ya Ubelgiji, Campbell, amejumuhishwa kikosini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img