12.7 C
New York

Simulizi (1): Patrick Kluivert; Aliua lakini familia ya marehemu ikamtetea asifungwe

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
PATRICK Kluivert, mzaliwa wa Jiji la Ajax, Uholanzi, alikulia katika familia ya wapenzi wa soka. Baba yake alicheza, ingawa hakufanikiwa kuwa mchezaji maarufu. Leo hii, mtoto wake, Patrick, ni staa kutokana na upekee wa kipaji alichokuwa nacho.
Kama ilivyokuwa kwa wengi waliojaa ndoto, Kluivert alianza safari yake ya kujifunza soka katika ‘academy’ maarufu ya Ajax katika miaka ya 1990.
Wakati huo, Ajax ilikuwa na kikosi cha hadhi kubwa si tu Ulaya, bali pia kilichozungumzwa duniani kote. Wachezaji kama Clarence Seedorf, Edgar Davids, Dennis Bergkamp, na George Weah.
Mwaka 1995, kikosi cha Ajax kilifikia kilele cha mafanikio kilipoingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan ya Italia.
Katika mchezo huo muhimu, Kluivert alifunga bao pekee na la ushindi, akiivua Milan ubingwa na kuwaweka Ajax kwenye ramani ya soka la dunia.
Alikuwa na umri wa miaka 18 tu wakati alipofunga bao hilo la kichwa, ambalo liliingia kwenye historia ya klabu hiyo na kumfanya kuwa shujaa wa Ajax.
Baada ya kutwaa kombe hilo la kihistoria, Kluivert, alipanda sana katika dunia ya soka, ingawa kama ilivyo kwa maisha ya wachezaji wengi, mafanikio ya uwanjani hayakukubaliana na maisha binafsi.
Miezi michache baadaye, wakati akiwa kwenye mapumziko, Kluivert alijikuta kwenye matatizo makubwa. Akiwa na rafiki yake ndani ya gari aina ya BMW, walipata ajali mbaya.
Mosi, gari halikuwa na bima. Pili, alikuwa akiendesha kwa mwendo mkali mitaani. Gari hilo likamgonga mzee mmoja na akafariki papo hapo, huku rafiki yake Kluivert akijeruhiwa vibaya.
Alipofikishwa mahakamani, Kluivert alikiri makosa (gari kukosa bima na kuendesha kwa mwendo mkali), hivyo akahukumiwa kifungo cha saa 360, pamoja na kufanya kazi za kijamii.
Cha kushangaza, hata familia ya marehemu (mzee aliyegongwa na gari) haikufurahishwa na hukumu hiyo. Ilitaka Kluivert asamehewe.
Wananchi wa Jiji la Amsterdam waliokusanyika nje ya Mahakama walibeba mabango mengi na moja lilisomeka: “Mmesahau juzi alitufanikishia kombe kupitia bao lake la kichwa?”
Hatimaye, Kluivert alimaliza adhabu yake ya gerezani na maisha yakaendelea. Safari ya soka haikuishia hapo.
Kluivert alisajiliwa na AC Milan mwaka 1997 lakini changamoto za kucheza Ligi kubwa zilimfanya ang’are mwaka mmoja baadaye, ambapo alikuwa mmoja ya wachezaji waliotumika zaidi klabuni hapo.
Ni baada ya kuwika zaidi, ndipo nyota yake ilioong’ara zaidi na kusajiliwa na vigogo wa La Liga, Barcelona, na kupata umaarufu mkubwa kuliko awali.
Alitua Ligi Kuu ya England aliposajiliwa na Newcastle United mwaka 2004, kabla ya kustaafu miaka minne baadaye akiwa LSK Lokeren ya Ubelgiji.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img