MERSEYSIDE, England
MLINDA mlango wa Liverpool, Alisson Becker, yuko kwenye hatua nzuri ya kujiunga na vigogo wa Serie A, Juventus.
Juventus wanampigia hesabu Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 33, licha ya kwamba bado ana mkataba na Juventus utakaokwisha mwaka 2027.
Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo ya Italia imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake ili atue jijini Turin mwishoni mwa msimu huu.
Inaelezwa kwamba Juventus wamempa ofa ya mkataba wa miaka miwili, pia kitakuwepo kipengele cha kuongezwa miezi 12.
Licha ya kuwa tayari ana Michele Di Gregorio na Mattia Perin, kocha wa Juventus, Luciano Spalletti, anaamini lango lao linahitaji uwezo na uzoefu wa Becker.


