20.5 C
New York

Rooney: Saka amerudi kuipa ubingwa Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Manchester United, Wayne Rooney, anaamini kurejea dimbani kwa Bukayo Saka kutaipa nguvu kubwa Arsenal katika mbio zake za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.

Baada ya muda mrefu wa kuuguza majeraha, Saka alicheza kwa mara ya kwanza wikiendi iliyopita, alipotokea benchi katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United.

Eberechi Eze ndiye aliyefunga bao pekee la Washika Bunduki, hivyo kurudisha pengo la pointi tatu na Manchester City inayoshika nafasi ya pili.

Akimzungumzia Saka, Rooney amesema: “Bukayo Saka amekuwa na mchango mkubwa mno kwa Arsenal kwa miaka michache ya hivi karibuni.

“Ni kweli huenda msimu huu hawaja fiti lakni bado ni mchezaji muhimu kwao. Hivyo, kurudi kwake ni jambo kubwa.”

Related articles

Recent articles