20.6 C
New York

Usiyoyajua kuhusu ‘playoff’ inayoisubiri DRC

Published:

LONDON, Uingereza
MACHI 31, mwakani, ndipo zitakapopatikana timu zote 48 zitakazoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika katika mataifa matatu; Marekani, Canada na Mexico.
Kufikia sasa, timu 42 zimeshajihakikishia nafasi ya kwenda kwenye mashindano hayo makubwa ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Je, ni timu zipi zilizobaki, zikisubiri hatua ya mchujo (playoff) kupata nafasi sita zilizobaki? Makala haya yanachambua, ikizingatiwa kuwa DRC ndiyo pekee kutoka Afrika inayowania nafasi.
Iko hivi; hatua ya ‘playoff’ imegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni la timu za Ulaya. Kundi jingine ni la timu za mabara mengine.
Kwa upande wa Ulaya, zimebaki nafasi nne za uwakilishi, wakati mabara mengine yana nafasi mbili zilizobaki.
Mataifa ya Ulaya yanayosubiri hatima ya nafasi nne hizo ni Albania, Bosnia, Czech, Denmark, Italia, Kosovo, Poland, Ireland, Slovakia, Uturuki, Ukraine, Wales, Romania, Sweden, Ireland ya Kaskazini na Macedonia.
Nafasi mbili kwa mabara mengine zinagombewa na Bolivia, DR Congo, Iraq, Jamaica, New Caledonia na Suriname.
Sasa, mechi za playoff zitachezwaje? Ni kwa namna gani makundi hayo yatapangwa ili kupata timu sita zilizobaki?
Kwa Ulaya, timu 16 zitagawiwa katika makundi manne. Katika kila kundi, kutakuwa na mechi mbili za nusu fainali, kisha mabingwa watacheza fainali ili kupata timu itakayokwenda Kombe la Dunia.
Kwa mabara mengine, ambapo zipo timu sita zinazowania nafasi mbili, DRC na Iraq zimeshasogea katika fainali ya playoff.
Hivyo, timu nne zilizobaki zitakutana katika nusu fainali, kisha zitazifuata Iraq na DRC kwa ajili ya mechi mbili za fainali zitakazoamua timu (2) za kwenda Kombe la Dunia.

Related articles

Recent articles