AMSTERDAM, Uholanzi
MABOSI wa klabu ya Ajax wako mbioni kumfuta kazi kocha John Heitinga, licha ya kwmaba ni miezi sita tu tangu ilipompa ajira ya kuliongoza benchi la ufundi.
Heitinga mwenye umri wa miaka 41, ameshinda mechi tano pekee kati ya 11 za Ligi Kuu ya Uholanzi na sasa Ajax imeachwa pointi nane na Feyenoord iliyokaa kileleni mwa msimamo.
Kwa upande wa Ligi ya Mabingwa, Ajax imepoteza mechi zote nne ilizocheza msimu huu, kikiwamo kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Galatasaray hivi karibuni.
Heitinga alitua Ajax akitokea Liverpool alikokuwa msaidizi wa Arne Slot wakati timu hiyo ikichukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu uliopita.
Beki huyo wa zamani wa Everton alisaini mkataba wa miaka miwili na Ajax, klabu ambayo aliwahi kucheza mechi zaidi ya 200.
Endapo atafukuzwa, basi hata msaidizi wake, Marcel Keizer, atalazimika kuondoka klabuni hapo na Fred Grim atashika kwa muda majukumu ya kukinoa kikosi.
Published:


