23.2 C
New York

Misri, Nigeria kuvaana Desemba 14

Published:

CAIRO, Misri
TIMU ya soka ya taifa ya Misri itaikabili Nigeria katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na fainali za mwaka huu za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mchezo huo wa ‘kutesti mitambo’ utachezwa Desemba 14 katika Uwanja wa Cairo, kwa mujibu wa Chama cha Soka cha Misri (EFA).
Ikumbukwe, Mafarao wamepangwa Kundi B, ambalo pia lina Afrika Kusini, Angola na Zimbabwe.
Taarifa zinaeleza kuwa kocha wa Misri, Hossam Hassan, aliwasilisha ombi kwa mabosi wa EFA akiwaambia anahitaji mechi moja dhidi ya timu kubwa barani Afrika.
Misri, ukiweka kando AFCON, pia wanakabiliwa na michuano ya Falme za Kiarabu, ambapo watashuka dimbani Novemba 14 kuivaa Uzbekistan.
Michuano hiyo pia inazishirikisha Cape Verde na Iran, ambazo pia zitatoana jasho muda mfupi kabla ya mchezo huo wa Misri.
Timu mbili zitakazopata ushindi zitacheza fainali inayotarajiwa kupigwa Novemba 18.
Awali, Senegal ilitarajiwa kushiriki mashindano hayo lakini ilijitoa, hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Cape Verde.

Related articles

Recent articles