MADRID, Hispania
KIUNGO wa Real Madrid, Jude Bellingham, amefunga bao moja na kutoa ‘asisti’ katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid.
Akifunga katika dakika ya 43, limekuwa ni bao la nne kwa Bellingham katika mechi tano za El Classico alizokutana na Barcelona.
Hata hivyo, ni kwa mara ya kwanza kiungo huyo amefunga na kutoa pasi ya bao tangu msimu huu wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) ulipoanza.
Bellingham alitoa asisti kwa Kylian Mbappe aliyeifungia Madrid bao la kuongoza katika dakika ya 22, kabla ya Fermin Lopez kuisawazishia Barcelona dakika tano baadaye.
Kwa upande mwingine, Madrid wangeweza kupata bao la penalti lakini mwamuzi alipotumia VAR alibaini kuwa Mbrazil huyo alijigonga kwenye mguu wa Lamine Yamal kabla ya kuanguka kwenye boksi.
Ni kwa ushindi huo, kikosi cha Madrid chini ya kocha Xabi Alonso kimekaa kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi tano .
Msimu uliopita ulikuwa mbaya kwa Madrid katika mechi za El Clasicos, ambapo ilipoteza zote nne mbele ya wapinzani wao wakubwa, Barcelona.
Published:


