ISTANBUL, Uturuki
STRAIKA wa kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen, jana alifunga mara mbili na kutoa ‘asisti’ katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bodo/Glimt.
Ni kwa maana hiyo, sasa Osimhen anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Galatasaray kupasia nyavu katika mechi saba mfululizo za Ligi ya Mabingwa.
Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifunga mabao yake kipindi cha kwanza, kabla ya asisti kwa Yunus Akgun baada ya timu hizo kurejea kipindi cha pili.
Kwa upande wake, Bodo/Glimt ya Ligi Kuu nchini Norway ilipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Andreas Helmersen aliyeingia akitokea benchi.
Hii inakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 kwa Galatasaray kushinda mechi mbili mfulululizo katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.
Published:


