VILLARREAL, Hispania
BAADA ya kuingia kambani mara moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Villarreal, Erling Haaland ameifikia rekodi ya Cristiano Ronaldo.
Haaland amezifumania nyavu katika mechi 12 mfululizo, kama alivyofanya Ronaldo akiwa na Real Madrid mwaka 2018.
Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, bao jingine la Manchester City lilipachikwa na kiungo Bernardo Silva.
Wakiwa katika Uwanja wa Estadio de la Ceramica, Man City walimaliza ukame wa miezi 12 wa kukosa ushindi katika mechi za ugenini.
Matokeo ya mechi zingine za Ligi ya Mabingwa barani Ulaya zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo;
Barcelona 6-1 Olympiacos, Arsenal 4-0 Atletico Madrid, Leverkusen 2-7 PSG, Newcastle United 3-0 Benfica, PSV 6-2 Napoli, Royal Union 0-4 Inter, Kairat Almaty 0-0 Pafos, na FC Copenhagen 2-4 Dortmund.
Published:


