LONDON, Uingereza
KLABU ya Nottingham Forest imemfuta kazi kocha wake raia wa Austria, Ange Postecoglou, akiwa amehudumu kwenye benchi la ufundi kwa siku 39 pekee.
Postecoglou anakuwa kocha wa pili katika historia ya Ligi Kuu ya England kudumu muda mfupi kazini baada ya Sam Allardyce, ambaye Leeds United walimfukuza ndani ya siku 30 tu.
Uamuzi wa Postecoglou kufukuzwa ulitangazwa dakika 19 tu baada ya mchezo wa Forest kufungwa mabao 3-0 na Chelsea.
Hata kabla ya filimbi ya mwisho ya mechi hiyo ya Ligi Kuu, mmiliki wa Forest, Evangelos Marinakis, alionekana akiondoka jukwaani.
Postecoglou mwenye umri wa miaka 60, ameondoka kwenye benchi la ufundi akiwa hajashinda hata mechi moja kati ya nane alizokaa kwenye benchi.
Published:


