23.5 C
New York

Maresca athibitisha Palmer nje wiki sita

Published:

LONDON, Uingereza
MKUU wa benchi la ufundi la Chelsea, Enzo Maresca, ameweka wazi kuwa atamkosa kwa wiki sita mshambuliaji wake tishio, Cole Palmer.
Palmer, raia wa England mwenye umri wa miaka 23, hajacheza mechi ya ushindani tangu Septemba 20, mwaka huu.
Kwa msimu huu, nyota huyo amecheza mechi tatu pekee za Ligi Kuu, hivyo ana nafasi finyu ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya Thomas Tuchel.
Awali, kocha Maresca alisema Palmer angerejea Novemba lakini amebadili uelekeo. “Sikuwa sahihi. Kwa bahati mbaya, atakuwa nje kwa wiki sita,” amesema kocha huyo.
“Tunajaribu kumlinda Cole kwa kadiri tunavyoweza. Muhimu zaidi si kurudi, bali kurudi akiwa fiti.”
Mshambuliaji huyo alikuwa mchezaji muhimu kwa Blues msimu uliopita, ambapo aliifungia mabao 15 kwenye mechi za Ligi Kuu pekee.
“Ni ngumu kuziba pengo la Cole, kwa sababu Cole ni mchezaji muhimu mno kwa upande wetu. Huenda ni mchezaji bora zaidi kwenye Ligi, hivyo si rahisi kuziba pengo lake,” amesisitiza Maresca.

Related articles

Recent articles