23.5 C
New York

Guardiola asema hajui kuhusu Rodri

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amekiri kuwa hafahamu siku atakayorudi uwanjani kiungo wake raia wa Hispania, Rodri.
Rodri (29), atakosekana katika mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Everton baada ya kupata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Brentford.
Mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka jana, alikosa mechi nyingi msimu uliopita kutokana na majeraha ya goti.
Rodri alikosa mechi ya kwanza ya msimu huu dhidi ya Wolves na ameshuka dimbani mara saba pekee kufikia hatua hii.
Kwa upande mwingine, habari njema kwa Guardiola ni kurejea kwa kiungo Mateo Kovacic, ambaye hajacheza hata mechi moja msimu huu.
Ni katika taarifa nyingine, inaelezwa kuwa nyota wawili, Omar Marmoush na Rayan Ait-Nouri, nao wameshaanza kufanya mazoezi na wenzao baada ya kupona majeraha.

Related articles

Recent articles