8.4 C
New York

Macho yote msimu ujao Ligi Kuu ya Uturuki

Published:

ISTANBUL, Uturuki
KUELEKEA msimu ujao, klabu za Ligi Kuu ya Uturuki zimeonekana kuvimbiana na zile za matajiri wa Saudi Arabia katika soko la usajili la majira haya ya kiangazi.
Klabu za Galatasaray, Fenerbahce na Besiktas zimeonesha jeuri ya fedha kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa barani Ulaya.
Mabingwa wa msimu uliopita, Galatasaray, hawakuona shida kuipa Napoli kitita cha euro milioni 75 kuinasa saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Victor Osimhen.
Kwa kiasi hicho, Osimhen anakuwa mchezaji wa bei mbaya zaidi katika historia ya soka la Uturuki, pia akishika nafasi ya nne duniani.
Galatasaray itakuwa ikimlipa mshahara wa euro milioni 21 kwa mwaka, huku Leroy Sane aliyesajiliwa na klabu hiyo akitokea Bayern Munich akikinga euro milioni 12.
Kwa upande wao, Fenerbahce wamekamilisha usajili wa mkopo wa straika wa Al-Nassr, Jhon Duran, ambaye mshahara wake ni euro milioni 20 kwa mwaka.
Duran anakutana na mchezaji mwingine aliyetokea katika klabu hiyo ya Al-Nassr, Anderson Talisca, ambaye Fenerbahce wanamlipa euro milioni 15.
Wakati huo huo, Beiktas inaye mshambuliaji wa zamani wa klabu za Chelsea na AS Roma, Tammy Abraham, ambaye mshahara wake ni euro milioni 10 kwa mwaka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img