28.7 C
New York

Anthony Taylor amestaafu kwa heshima, alinusurika kichapo

Published:

LONDON, Uingereza

BAADA ya miaka 20 ya kufanya kazi, akichezesha mechi 831, mwamuzi wa kati raia wa England, Anthony Taylor, alitangaza kustaafu hivi karibuni.

Mechi yake ya mwisho ni ile ya hatua ya 16 Bora ya msimu huu wa Kombe la Dunia, ambapo Hispania iliifunga Ureno bao 1-0 na kutinga robo fainali.

MECHI ZAIDI YA 400 EPL

Taylor (47), alianza kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya England (EPL) mwaka 2010 (Fulham 1-0 Portsmouth). Tangu hapo, amepuliza kipyenga katika mechi 432 za Ligi Kuu hiyo.

Kwa ujumla, Taylor analiacha soka akiwa amesimama katikati ya uwanja katika mechi 668 za ndani ya England.

MECHI ZA KIMATAIFA

Tangu alipopata beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) miaka 14 iliyopita, Taylor amechezesha mechi za kimataifa 163, akishiriki mara mbili Kombe la Dunia (2022 na 2026).

Pia, refa huyo ameshiriki mara mbili fainali za Mataifa ya Ulaya (EURO);
na EURO mara mbili (2020 na 2024).

SIASA ZILIMNYIMA FAINALI

Kama itakumbukwa, ilikuwa mwaka 2022, wakati wa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini Qatar.

Taylor aliteuliwa kuchezesha fainali kati ya Argentina na Ufaransa, lakini FIFA ilimtoa baadaye na nafasi yake kuchukuliwa na refa mwingine.

Uamuzi wa kumtoa ulitokana na uhusiano mbaya wa kisiasa uliopo kati ya nchi yake (England) na Argentina.

REKODI YA KADI

Mei 31, 2023, Taylor alichezesha fainali ya Ligi ya Europa kati ya AS Roma na Sevilla. Alitoa kadi za njano 14 na kuwa kocha wa kwanza katika historia ya michuano hiyo kufikisha idadi hiyo kwenye mchezo mmoja.

Moja ya kadi hizo alimlima Jose Mourinho, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa benchi la ufundi la Roma ya Ligi Kuu nchini Italia.

Septemba 14, 2024, Taylor alikuwa uwanjani kuchezesha mechi ya EPL kati ya Chelsea na Bournemouth.

Katika mchezo huo, pia alitoa kadi za njano 14 na kuwa refa wa kwanza kufikisha idadi hiyo katika mchezo mmoja wa Ligi Kuu hiyo.

ANUSURIKA KICHAPO

Kama ilivyoelezwa awali, mechi ya fainali ya Ligi ya Europa kati ya Roma na Sevilla iliyochezwa Mei 31, 2026, ilikuwa na presha kubwa, hivyo Taylor kutembeza kadi za njano 14.

Kwa mashabiki wa Roma, ilikuwa siku mbaya zaidi. Kabla ya kocha wao, Mourinho, kupewa kadi ya njano, Taylor aliipa penalti Sevilla, kabla ya VAR kuifuta.

Katika dakika ya 81, Taylor aliwanyima Roma mkwaju wa penalti baada ya Fernando wa Sevilla kugusa kwa mkono mpira wa ndani ya boksi.

Baada ya mechi, Mourinho na Taylor walikaribia kupigana walipokutana katika maegesho ya magari.

Pia, Taylor na familia yake wakiwa uwanja wa ndege walikaribia kupigwa na mashabiki wa Roma lakini polisi waliingilia kati na kuwasindikiza kwa ulinzi.

Baadaye, alikiri kuwa Mourinho alichangia hasira za mashabiki hao, pia akiongeza kuwa familia yake imeacha kwenda viwanjani baada ya tukio hilo.

Related articles

Recent articles