8.9 C
New York

Watetezi wa haki za watoto wapewa mafunzo ya kuimarisha ushiriki kimataifa

Published:

Na Nora Damian, Gazetini

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha mafunzo maalum kwa Watetezi wa Haki za Watoto, yakilenga kuwaongezea ujuzi na nyenzo za kutatua changamoto za haki za watoto na kukuza ushiriki wao katika mifumo ya haki za binadamu ya kikanda na kimataifa.

Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utetezi wa THRDC, Wakili Paul Kisabo, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada endelevu za kuwawezesha watetezi kushirikiana na Serikali katika kulinda haki na ustawi wa watoto.

“Mafunzo haya yatawasaidia Watetezi wa Haki za Watoto kushiriki kikamilifu kwenye mifumo ya haki za binadamu ya kimataifa na kikanda, kuongeza ubora wa ripoti, na kushawishi utekelezaji wa mapendekezo,” amesema Kisabo.

Alitaja changamoto kubwa zinazowakabili watetezi hao kuwa ni ukosefu wa uelewa, ujuzi mdogo wa kuandaa ripoti mbadala, na ushirikiano hafifu katika kufuatilia mapendekezo. THRDC inalenga kuziba mapengo hayo kwa mafunzo endelevu ili kuimarisha sauti ya Watetezi wa Haki za Watoto nchini na kulinda mustakabali wa mtoto.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img