21.8 C
New York

Mahrez saini yake dili Serie A

Published:

MILAN, Italia

JINA la winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, limeingia kwenye rada za mabosi wa klabu kubwa za Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Nyota huyo wa zamani wa Manchester City ameshaondoka Al-Ahli ya Saudi Arabia baada ya makubaliano ya pande mbili.

Akiwa na umri wa miaka 35, bado Mahrez anajiona ana nafasi katika soka la Ulaya na klabu za Serie A ndizo zinazoiwania saini yake.

AS Roma ni miongoni mwa zinazomtolea macho, licha ya kuwa na Paulo Dybala na Matias Soule katika eneo hilo la winga wa kulia.

Wakati huo huo, ripoti zinaeleza kuwa Juventus imejitosa kuiwania saini ya Mahrez. Vigogo hao wa Turin wako tayari kumuuza Lois Openda ili kufanikisha dili hilo.

Inter Milan nayo inamtaka, kama ilivyo kwa Como ya kocha Cesc Fabregas, ambaye huenda akampoteza Alvaro Morata kipindi hiki cha kiangazi.

Wakati huo huo, klabu za AC Milan na Napoli nazo zinatajwa na vyanzo kadhaa vya habari, kwamba zinampigia hesabu Mahrez.

Related articles

Recent articles